Vitabu sahili

LoGo

Elimu kubwa isiyo na mwisho inapatikana katika vitabu. Soma vitabu na elimika. Wote waandishi na waandikiwa wanakutanishwa hapa. Pata elimu hazina isiyoharibika hapa.

GO_HOME
Ijue Mimeadawa ya Tiba & Huduma ya Kwanza
DIBAJI.
Kijitabu hiki, Ijue Mimeadawa ya Tiba & Huduma ya Kwanza, nimekiandika ili kiweze kuwa cha msaada katika kutatulia matatizo yawezayo kumpata mtu akiwa amezungukwa na mimea iwezayo kumsaidia. Bila kujua mtu aweza kutaabishwa na tatizo dogo tu akaacha shughuli zake kufuata huduma ya kuzuia au kumwondolea maumivu fulani.
Msomaji wa kitabu hiki anaalikwa kukisoma ili kujipatia ujuzi wa vitu mbalimbali viwezavyo kumsaidia katika kutatulia baadhi ya matatizo yawezayo kujitokeza katika mazingira yake
......Nakitoa pia kwa heshima ya Marehemu mama yangu, Salome Nkomanyiwa Idimulwa, niliyemwona utotoni akiwaogesha wadogo zangu kwa maji alimoloweka mizizi ya Strophanthus eminii (Nsungululu –Kisukuma). Kutokana na kujionea mmea huo ulivyofanya ngozi kuwa laini na nyororo bila vipele; niliamua kuujaribu utomvu wa jani la Strophanthus kudondoshea kwenye jeraha langu nalo lilipona kirahisi ukawa mwanzo wa kuutumia utomvu huo kwa majeraha yangu na wengine niliopata kuwashauri kutumia...
Alfonsi S MAHUYEMBA 0754031284
Kwa maswali na maelezo zaidi tumia barua-pepe bidhaa@sahili.net )

 • gamba

 • Nahitaji softcopy
  Kitabu chenyewe ( tsh)
  Mahali ulipo/mji
  Email
  Namba ya simu
  Idadi ya kopi


  Zijue Mboga-pori na Manufaa Yake
  DIBAJI.
  Kijitabu hiki, Zijue Mboga-pori na Manufaa Yake, kinatarajiwa kuwafaa wale wote wapendao kula mboga za majani.
  Kitawaongezea chaguo.
  Pamoja na zile zistawishwazo bustanini zenye kuchumwa toka misituni zaweza kunufaisha walaji wake kilishe kwa vile zina viinilishe asilia bila kemikali amabazo baadhi hushukiwa kuathiri afya ya mlaji hasa ikiwa zimetumiwa kiholela!
  Ujio wa Wageni katika nchi yoyote huleta ‘usitaarabu’ wa kigeni ambao huleta mabadiliko katika mitindo ya maisha na lishe ya wenyeji: mabadiliko katika namna ya kuishi na kula (lishe) hayawezi kutokea bila kumwathiri muhusika kiafya pia.
  Wageni walikuja na mboga za majani wazipendazo. Waliwakuta wenyeji na mboga zao za asili; walizostawisha mashambani na bustanini, na; hapo awali walizijua na kuzichuma zile za porini wakazipika.
  Uchanganyikaji na wageni na uhamiaji mijini baadaye ulianza kuibadili mitazamo ya wenyeji na kuanza kutothamini baadhi ya kile walichokuwa nacho wakakienzi. Badala ya kuboresha vya kwao kiasili watu walianza kuachana navyo!
  Alfonsi S MAHUYEMBA 0754031284
  Kwa maswali na maelezo zaidi tumia barua-pepe bidhaa@sahili.net )

 • gamba

 • Nahitaji softcopy
  Kitabu chenyewe(Kinaandaliwa)
  Mahali ulipo/mji
  Email
  Namba ya simu
  Idadi ya kopi


  Taarifa zilizo katika mtandao huu hazilengi kuwa mbadala wa taarifa rasmi kutoka katika vyombo vyenye mamlaka kama, daktari au mtoa huduma ya afya. Au sekta yoyote rasmi. Taarifa na habari hizi ni kwa ajili ya ujuzi tu.