tafiti sahili

LoGo

Uchunguzi wa uelewa na ufanyaji wa uchunguzi binafsi wa matiti kati ya wanafunzi wa kike katika Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili.

Agripina Gotfrid Massawe


Assessment of Knowledge and Practice of Breast Self-Examination Among Female Undergraduate Student at MUHAS, Dar es Salaam, Tanzania.

Muhtasari

Ugundulikaji wa haraka wa kansa ya matiti kwenye jamii kupitia program ya uchunguzi binafsi wa matiti umekuwa muhimu katika kupunguza kansa na vifo vitokanavyo na kansa ya matiti. Uchunguzi binafsi wa matiti umekuwa njia nzuri ya kuepusha vifo hivyo kwa sababu husaidia kugundua na kutibu mapema.

Dhumuni
Kuchunguza uelewa na ufanyaji wa uchunguzi binafsi wa matiti kati ya wanafunzi wa kike ngazi ya Shahada katika Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili.

4. Mamlaka
Mtafiti: Agripina Gotfrid Massawe
Mthibiti:Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)
Matakwa binafsi: Sina matakwa binafsi

5. Mbinu na namna ulivyofanyika
Tafiti hii iifanyika kati ya mwezi Disemba, 2017 na mwezi wa tatu, 2018 kati ya wanafunzi 101 wa kike ngazi ya shahada katika Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Dar es Salaam, Tanzania. Maswali 15 mafupi yaliyoandaliwa na kupewa kwa washiriki yalitumika kukusanya taarifa binafsi ,uelewa na ufanyaji wa uchunguzi binafsi wa matiti. Pia wanafunzi waliangaliwa namna wanavyojifanyia uchunguzi wa matiti wenyewe na taarifa zao zilijazwa katika fomu maalumu iliyoandaliwa.

6. Matokeo
Jumla ya wanafunzi 101 walishiriki kwenye tafiti.Wengi 67 (66.3%) walikuwa na uelewa mkubwa,28 (27.7%) walikuwa na uelewa wa kati na 6 (5.9%) walikuwa n uelewa mdogo na wengine hawakuwa na uelewa kabisa kuhusu uchunguzi Binafsi wa matiti.5(5%) walikuwa na ufanyaji mzuri,46 (45.5%) walikuwa na ufanyaji wa kati na 50 (49.5%) hawakujua kufanya uchunguzi wa matiti.Hakukuwa na uhusiano kati ya uelewa na ufanyaji wa uchunguzi binafsi wa matiti na hii ilithibitishwa na thamani ya P=0.287 katika mwendano wa asilimia 95.

7. Hitimisho na Pendekezo
Ili kuimarisha ufanyaji wa uchunguzi binafsi wa matiti, ni muhimu kuhakikisha kuwa wafanyakazi wa afya kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali wanaimarisha mazingira ya kazi pamoja na kuwaelimisha wanawake katika umuhimu wa kufanya uchunguzi binafsi wa matiti katika nchi yetu, Tanzania.

8. Maandishi ya kurejea
Utangulizi wa kiingereza unapatikana hapa Abstract; Assessment of Knowledge and Practice of Breast Self-Examination Among Female Undergraduate Student at MUHAS, Dar es Salaam, Tanzania.


Www.free-counter-plus.com

Waionaje tafiti hii (Maoni)
Sahili__ni rahisi na inaeleweka
Tata__ ni ngumu kueleweka
Nzuri__inafaa kwa ajili ya wanadamu
Maoni kwa ufupi

Taarifa zilizo katika mtandao huu hazilengi kuwa mbadala wa taarifa rasmi kutoka katika vyombo vyenye mamlaka kama, daktari au mtoa huduma ya afya. Au sekta yoyote rasmi. Taarifa na habari hizi ni kwa ajili ya ujuzi tu.