tafiti sahili

LoGo

Matumizi ya malimao na athari zake katika kasi ya uondoshwaji wa vijidudu vya malaria na hali ya damu ya panya walioambukizwa P. berghei.

Kelvin Mashauri Shija


Effect of lemon decoction on malaria parasite clearance and selected hematological parameters in Plasmodium berghei infected mice.

Muhtasari

Limao ni tunda litokanalo na mlimao. Mlimao hupatikana katika familia ya Rutacea katika kundi la Citrus, ni mmea uliosambaa ulimwenguni kote
Matunda haya hutumika kama chakula, kutia ladha, juisi na katika mapishi mbalimbali. Matumizi ya malimao hayakuishia hapo, watu huyatumia katika matibabu ya saratani, uzito (unene), pamoja na malaria ki-jadi.
Tafiti zimeonesha matokeo mazuri katika vipimo vya damu kutokana na matumizi ya limao au sehemu zake.Lakini hata hivyo baadhi ya wanajamii wamekuwa na imani ambayo haikuthibitishwa.
Katika utafiti mmoja matumizi ya juisi ya ndimu pamoja na dawa mseto za malaria yalipelekea matokeo mazuri katika matibabu ya malaria. Katika jamii malimao huchemshwa na kutumika katika matibabu ya malaria. Utafiti katika matumizi hayo ni wa kuripotiwa na mtu mmojammoja hivyo utafiti huu unaangazia uthabiti wa matumizi hayo.

Kusudi
Kuchunguza madhara ya malimao katika kupambana na malaria pamoja na athari zake kati hali ya damu kwa ujumla, utafiti uliofanywa kwa panya walioambukizwa vijidudu vya Plasmodium berghei.


4. Mamlaka
Mtafiti: Kelvin M. Shija
Mthibiti:Chuo cha afya na sayansi shirikishi MUHIMBILI (MUHAS)
Matakwa binafsi: Sina matakwa binafsi.

5. Mbinu na namna ulivyofanyika
Vipande vya limao vilikatwakatwa na kisha kuongezewa maji na kuchemshwa kwa muda wa dakika 45. Kila siku mchanganyiko mpya ulitengenezwa. Panya 25 walitumika katika utafiti huu.
Mtindo wa utafiti alioutumia Ryley na mwenzake Peters uitwao 'Kipimo cha matibabu cha Rane' ulitumika. Panya 20 waliambukizwa na malaria kisha baada ya muda waligawanywa katika makundi manne ya matibabu
1. Walipewa maji tu
2. Walipewa mchemsho wa malimao
3. Walipewa dawa mseto
4. Walipewa limao pamoja na dawa mseto
5. Hawa hawakuambukizwa wala kutibiwa (uangalizi)
Matibabu yalifanywa kwa muda wa siku nne. Vipimo vya malaria vilifanyika kila siku kwa siku tano. Damu ilipimwa kwa kuangalia wingi wa damu na seli nyinginezo kwa mashine maalumu. Kwa baadhi ya makundi wingi wa damu ulipimwa kwa kutumia njia rahisi ya mashine izungukayo.

6. Matokeo
Katika siku ya nne ya matibabu vipimo vilionesha kuwa; kwa wastani wadudu katika kundi lililopewa malimao walikuwa wachache (24%) ukilinganisha na kundi ambalo hawakutibiwa kabisa (40%)
Lakini kundi lililopewa dawa mseto ndilo halikuwa na wadudu kabisa (0%)
Siku za kuishi pia ziliongezeka katika kundi lililopewa malimao (siku 11) ukilinganisha na kundi ambalo hawakutibiwa (siku 8)
Katika vipimo vya damu hakukuwa na utofauti wa kutokana na matumizi ya malimao ulioweza kujipambanua kitakwimu
. Hata hivyo matumizi ya malimao kwa pamoja na dawa mseto yalipelekea kupunguza muda uliohitajika kuondosha asilimia 99% ya vijidudu vya malaria ukilinganisha na kutumia dawa mseto peke yake. (saa 58.8 vs saa 62.2). Tofauti hazikuonekana kuwa kubwa katika uzito wa panya kutokana na matumizi ya malimao

8. Mchanganuo na majadiliano
Utafiti huu japo umefanyika katika panya, lakini umeonesha matokeo yanayotufungua bongo katika matumizi ya malimao
Kuongezeka kwa kasi ya kuondoshwa kwa seli zilizoathiriwa na malaria kunasemekana kuwa msingi wa matokeo haya.
Ukihitaji maelezo zaidi utayapata katika utafiti kamili ambao utachapishwa siku za usoni

Lakini utafiti wa mtu mmoja (Nimejifanya mnyama wangu wa majar..) unaweza kuupata hapa Makala

Hitimisho
Mchemsho huu wa malimao umeonesha kuwa na vitu vinavyosaidia kufubaza malaria kwa asilimia 39% ukilinganisha na panya wasiopewa dawa. Lakini haikutosha kuleta uponyaji kabisa mchemsho ulipotumika peke yake, malimao hayakuwakinga panya na upungufu wa damu utokanao na malaria. Lakini mchemsho wa malimao huohuo ulipotumika pamoja na dawa mseto matokeo mazuri zaidi yalipatikana kwa upande wa uondoshaji wa haraka wa vijidudu vya malaria na hali nzuri ya damu na kinga kwa ujumla.

9. Mapendekezo
Utafiti zaidi ufanyike kwa binadamu waishio maeneo yenye malaria (endemic) ili kuondoa tofauti zilizopo kati ya viumbe na namna asili ya ugonjwa ulivyo. Tafiti katika panya zina changamoto nyingi.

10. Maandishi ya kurejea
Utangulizi wa kiingereza hapa Abstract; Effect of lemon decoction on malaria parasite clearance and selected hematological parameters in plasmodium bhergei infected mice.
Marejeo mengine
1. Marejeo yapo katika utafiti mwenyewe


Http://www.free-counter-plus.com
Waionaje tafiti hii (Maoni)
Sahili__ni rahisi na inaeleweka
Tata__ ni ngumu kueleweka
Nzuri__inafaa kwa ajili ya wanadamu
Maoni kwa ufupi

Taarifa zilizo katika mtandao huu hazilengi kuwa mbadala wa taarifa rasmi kutoka katika vyombo vyenye mamlaka kama, daktari au mtoa huduma ya afya. Au sekta yoyote rasmi. Taarifa na habari hizi ni kwa ajili ya ujuzi tu.