tafiti sahili

LoGo

Nimejifanya Mnyama Wangu wa Majaribio Katika Kutibu Malaria

Alphonse Shija Mahuyemba


I am my own guinea pig in malaria remedying
Muhtasari Klorokwini ilishindwa kuponesha malaria. Dawa za SP zilisababisha mapigo ya moyo ya kasi isivyo kawaida. Kwa hali hiyo mwandishi wa mada hii (ndiye mnyama wa majaribio) aliamua kunywa dawa itokanayo na mmea ambayo ilisifiwa huponesha malaria.
Mwandishi huyu (mnyama wa majaribio) alipatwa na dalili zilizothibitika kwa hadubini kuwa ni ugonjwa wa malaria mara tatu. Safari zote hizo 3 mwandishi huyu alikunywa dawa iliyotokana na kuchemsha malimao (Citrus limon), juisi yake ilipopoa ilichanganywa na asali mbichi. Kila baada ya kujitibu kwa dawa hii wadudu wa malaria hawakuwa wakionekana kwenye damu ilipopimwa siku 4 au 11 baadaye.


2. Utangulizi
Klorokwini ambayo imekuwa ikinitibu tatizo la malaria tangu mwanzo lakini kama utani ilishindwa kunitibu tena. Hiyo ilikuwa ni July 2000. Nilipewa Fansidar. Mwaka mmoja baadae, nilipatiwa dawa nyingine ya mtindo wa SP nilipokutwa na malaria (2 ring forms/200BC)
Ile SP ilinitibu lakini nilipatwa na tatizo. Siku chache baadae moyo wangu ulikuwa ukidunda kwa namna isiyo ya kawaida. Hii ilinifanya kuhisi kuwa nimepatwa na haya kutokana na madhara pacha ya dawa hizi za SP (Falcidin, Fansidar,, Laridox, Malostat, Orodar na Metakelfin) kwangu.

Nilipokuja kuugua mara nyingine tena nilisita kuzitumia dawa hizohizo kutoka kwa matabibu waliokuwa wakigawa SP kwangu. Hapo ndipo nilipomkumbuka ndugu yangu (Mr. Emamanuel Mlimandago) aliyewahi kuelekeza matibabu ya mitishamba yenye uwezo wa kutibu malaria.

4. Mamlaka
Mtafiti:Alphonse S. Mahuyemba S.L.P 195 Kahama
Mthibiti:Binafsi
Matakwa binafsi: Sina matakwa binafsi.

5. Mbinu na namna ulivyofanyika
Kutengeneza juisi hii malimao (Citrus limon)matatu huchukuliwa na kusafishwa vizuri
Kisha hukatwakatwa vipande vinne kila moja. Vipande 12 vilivyopatikana huwekwa katika lita 1 na robo ya maji mchanganiko huu ukiishachemka hutokoswa kwa muda wa dakika 12 kisha huipuliwa.
Mchanganyiko ukiishapoa huchujwa kupata juisi safi.
Dozi ya dawa hii ni glasi moja iliyojaa ya juisi huchanganywa na kijiko kimoja cha asali kuchanganywa vizuri kisha hunywewa. Mchanganyiko huu hutumika mara tatu kwa siku
Kila mara mchanganyiko mpya wa dawa huandaliwa mara tu iliyotangulia ikiisha. Kwa wastani ni kila siku mchanganyiko mpya.


6. Matokeo
Matokeo yameoneshwa katika jedwali lifuatalo
MARA YA KWANZA
Tarehe Siku Kazi iliyofanyika Maoni
27/8/2002 Siku ya 0 Kupima malaria 2rings/200WBC
Siku ya 1 Kuandaa dawa/kunywa Glasi 1X3
Siku ya 2 '' ''
Siku ya 3 '' ''
Siku ya 7 Kupima malaria tena Wadudu wachache wameonekana
Siku ya 14 '' Malaria haikuonekana (0ring/200WBC)
MARA YA PILI
28/2/2003 Siku ya 0 Kupima malaria 2rings/200WBC
Siku ya 1 Kuandaa dawa/kunywa Glasi 1X3
Siku ya 2 '' ''
Siku ya 3 '' ''
MARA YA TATU
15/10/2003 Siku ya 0 (a.)Kupima malaria
(b.)Kuandaa dawa/kunywa
Glasi 1X2
Siku ya 1 Kuandaa dawa/kunywa Glasi 1X3
Siku ya 2 Kuandaa dawa/kunywa Glasi 0.5(nusu)X3
Siku ya 3 Kuandaa dawa/kunywa Glasi 0.5(nusu)X1
Siku ya 7 Kupima malaria 0ring/100WBC


Mchanganuo na majadiliano
Kwa kuwa mimi si mtaalamu sana wa mambo ya kitabibu sifahamu kwa undani ni nini hasa hufanyika hadi kutoa matokeo ya BS examination (kipimo cha malaria). Kwangu iaonekana kuwa sahihi kusema kwamba malaria husemekana kuwa ipo pale ambapo 'ring forms' wa malaria wanapoonekana katika damu ya mgonjwa.
Pale ambapo hakuna ring forms hizo katika damu ndiyo sawa na kusema hakuna wadudu wa malaria wanaoonekana katika damu.
Hivyo basi hiyo inanipa haki ya kusema kuwa mchanganyiko huu wa dawa (CILI extract) umeimaliza malaria kabisa katika sehemu tatu zilizooneshwa na matokeo.
Matukio ya kushambuliwa na malaria yametokea katika wilaya mbili tofauti, Kahama (Mara mbili) na Shinyanga (Mara moja). Malimao yaliyotumika Kahama ni yale yaliyokomaa na yale yaliyotumika Shinyanga yalikuwa machanga.
Dozi iliyotumika shinyanga ilianza mchana mara baada ya kupima na kugundulika kuwa na viini vya malaria. Ilianza saa kumi mchana na ya pili ilinywewa saa tano usiku.

Tatizo la kuharisha lilijitokeza siku ya pili ya kunywa dawa nikiwa Shinyanga. Baada ya kuhisi kuwa inawezekana ni kwa sababu ninatumia malimao machanga dozi ilipunguzwa hadi kufikia nusu kikombe. (Nusu kikombe cha juisi na kijiko kimoja cha asali mara tatu kwa siku). Kuharisha kulikoma. Na siku ya mwisho (Ya nne) nilimalizia dozi moja ya mwisho kukamilisha jumla ambayo ni mara tisa (9).
Na nilipona malaria.
Kupona kutokana na matumizi ya mchanganyiko huu inaweza kuwa labda ni faida ya chakula kikitumika vizuri kama dawa. Hivyo haitarajiwi kama inaweza kuwa na madhara makubwa sana (side effects).
Malimao hutumika katika mapishi mbalimbali (Katende na wenzie, 1995). Napia mchanganyiko wa malimao na juisi ni hutumika kwa ukawaida kuandaa nyama na samaki katika kile kinachoitwa 'marinating' (Malolo na wenzie, 2001).
Hata hivyo tuchukue tahadhari maana kuna usemi wa kiingereza usemao 'The safest medicine is only a useless one'. Uwezo wa dawa hii kuua vimelea vya malaria unatupa mwanya wa kufanya tafiti zaidi ili kuweza kupata dozi ambayo itaua wadudu tu bila madhara yeyote kwa mwili wa mwanadamu

Maumivu ya kichwa ambayo mara nyingi huambatana na homa ya malaria iliendelea kuwepo hadi siku ya pili na tatu za kutumia mchanganyiko wa dawa hii.

8. Hitimisho na mapendekezo
Kwa kukosa vifaa vya kisasa kuweza kufanya utafiti kimaabara. Msimuliaji anatarajia kuwa baadhi ya wasomaji wa utafiti/makala haya wataifanyia kazi kisayansi zaidi.

10. Maandishi ya kurejea
Tafiti ya kiingereza hapa I am my own guinea pig in malaria remedying
1. KATENDE,A.B,BIRNIE ANN; TEGNAS BO. (1995). Citrus limon Rutaceae. In : Useful Trees and Shrubs for Uganda
2. MALOLO,M.; MATENGA-SMITH,T.; TUNIDAU-SCHULTZ. J. 2001 Lemon Citrus limon In: The Fruits We Eat. SPC.CTA. Noumea, New Caledonia pp 46-49
Marejeo mengine

Soma kitabu chenye dawa zaidi hapa Ijue mimeadawa ya tiba na huduma ya kwanza


Free-counter-plus.com

Waionaje tafiti hii (Maoni)
Sahili__ni rahisi na inaeleweka
Tata__ ni ngumu kueleweka
Nzuri__inafaa kwa ajili ya wanadamu
Maoni kwa ufupi

Taarifa zilizo katika mtandao huu hazilengi kuwa mbadala wa taarifa rasmi kutoka katika vyombo vyenye mamlaka kama, daktari au mtoa huduma ya afya. Au sekta yoyote rasmi. Taarifa na habari hizi ni kwa ajili ya ujuzi tu.