tafiti sahili

LoGo

Tafiti zilizofanyiwa kazi na kupatikana majibu utazipata hapa. Mkusanyiko wa tafiti kutoka taasisi mbalimbali za kijamii na kielimu. Zote zikiwa na lengo la kuvumbua ujuzi ama kutoa ujumbe fulani kwa wanaadamu. Unaweza kutuma utafiti wako na kuchapisha hapa pia.

GO_HOME

Tafiti Zilizochapishwa

Naam zilizopata kuandikwa; Kufungua bofya 'soma zaidi' iliyo kushoto

Nimejifanya Mnyama Wangu wa Majaribio Katika Kutibu Malaria
Muhtasari Klorokwini ilishindwa kuponesha malaria. Dawa za SP zilisababisha mapigo ya moyo ya kasi isivyo kawaida. Kwa hali hiyo mwandishi wa mada hii (ndiye mnyama wa majaribio) aliamua kunywa dawa itokanayo na mmea ambayo ilisifiwa huponesha malaria.
Mwandishi huyu (mnyama wa majaribio) alipatwa na dalili zilizothibitika kwa hadubini kuwa ni ugonjwa wa malaria mara tatu. Safari zote hizo 3 mwandishi huyu alikunywa dawa iliyotokana na kuchemsha malimao (Citrus limon), juisi yake ilipopoa ilichanganywa na asali mbichi. Kila baada ya kujitibu kwa dawa hii wadudu wa malaria hawakuwa wakionekana kwenye damu ilipopimwa siku 4 au 11 baadaye.


2. Utangulizi
Klorokwini ambayo imekuwa ikinitibu tatizo la malaria tangu mwanzo lakini kama utani ilishindwa kunitibu tena. Hiyo ilikuwa ni July 2000. Nilipewa Fansidar. Mwaka mmoja baadae, nilipatiwa dawa nyingine ya mtindo wa SP nilipokutwa na malaria (2 ring forms/200BC)
Ile SP ilinitibu lakini nilipatwa na tatizo. Siku chache baadae moyo wangu ulikuwa ukidunda kwa namna isiyo ya kawaida. Hii ilinifanya kuhisi kuwa nimepatwa na haya kutokana na madhara pacha ya dawa hizi za SP (Falcidin, Fansidar,, Laridox, Malostat, Orodar na Metakelfin) kwangu.

Nilipokuja kuugua mara nyingine tena nilisita kuzitumia dawa hizohizo kutoka kwa matabibu waliokuwa wakigawa SP kwangu. Hapo ndipo nilipomkumbuka ndugu yangu (Mr. Emamanuel Mlimandago) aliyewahi kuelekeza matibabu ya mitishamba yenye uwezo wa kutibu malaria.

4. Mamlaka
Mtafiti:Alphonse S. Mahuyemba S.L.P 195 Kahama
Mthibiti:Binafsi
Matakwa binafsi: Sina matakwa binafsi.

5. Mbinu na namna ulivyofanyika
Kutengeneza juisi hii malimao (Citrus limon)matatu huchukuliwa na kusafishwa vizuri
Kisha hukatwakatwa vipande vinne kila moja. Vipande 12 vilivyopatikana huwekwa katika lita 1 na robo ya maji mchanganiko huu ukiishachemka hutokoswa kwa muda wa dakika 12 kisha huipuliwa.
Mchanganyiko ukiishapoa huchujwa kupata juisi safi.
Dozi ya dawa hii ni glasi moja iliyojaa ya juisi huchanganywa na kijiko kimoja cha asali kuchanganywa vizuri kisha hunywewa. Mchanganyiko huu hutumika mara tatu kwa siku
Kila mara mchanganyiko mpya wa dawa huandaliwa mara tu iliyotangulia ikiisha. Kwa wastani ni kila siku mchanganyiko mpya.


6. Matokeo
Matokeo yameoneshwa katika jedwali lifuatalo
MARA YA KWANZA
Tarehe Siku Kazi iliyofanyika Maoni
27/8/2002 Siku ya 0 Kupima malaria 2rings/200WBC
Siku ya 1 Kuandaa dawa/kunywa Glasi 1X3
Siku ya 2 '' ''
Siku ya 3 '' ''
Siku ya 7 Kupima malaria tena Wadudu wachache wameonekana
Siku ya 14 '' Malaria haikuonekana (0ring/200WBC)
MARA YA PILI
28/2/2003 Siku ya 0 Kupima malaria 2rings/200WBC
Siku ya 1 Kuandaa dawa/kunywa Glasi 1X3
Siku ya 2 '' ''
Siku ya 3 '' ''
MARA YA TATU
15/10/2003 Siku ya 0 (a.)Kupima malaria
(b.)Kuandaa dawa/kunywa
Glasi 1X2
Siku ya 1 Kuandaa dawa/kunywa Glasi 1X3
Siku ya 2 Kuandaa dawa/kunywa Glasi 0.5(nusu)X3
Siku ya 3 Kuandaa dawa/kunywa Glasi 0.5(nusu)X1
Siku ya 7 Kupima malaria 0ring/100WBC


Mchanganuo na majadiliano
Kwa kuwa mimi si mtaalamu sana wa mambo ya kitabibu sifahamu kwa undani ni nini hasa hufanyika hadi kutoa matokeo ya BS examination (kipimo cha malaria). Kwangu iaonekana kuwa sahihi kusema kwamba malaria husemekana kuwa ipo pale ambapo 'ring forms' wa malaria wanapoonekana katika damu ya mgonjwa.
Pale ambapo hakuna ring forms hizo katika damu ndiyo sawa na kusema hakuna wadudu wa malaria wanaoonekana katika damu.
Hivyo basi hiyo inanipa haki ya kusema kuwa mchanganyiko huu wa dawa (CILI extract) umeimaliza malaria kabisa katika sehemu tatu zilizooneshwa na matokeo.
Matukio ya kushambuliwa na malaria yametokea katika wilaya mbili tofauti, Kahama (Mara mbili) na Shinyanga (Mara moja). Malimao yaliyotumika Kahama ni yale yaliyokomaa na yale yaliyotumika Shinyanga yalikuwa machanga.
Dozi iliyotumika shinyanga ilianza mchana mara baada ya kupima na kugundulika kuwa na viini vya malaria. Ilianza saa kumi mchana na ya pili ilinywewa saa tano usiku.

Tatizo la kuharisha lilijitokeza siku ya pili ya kunywa dawa nikiwa Shinyanga. Baada ya kuhisi kuwa inawezekana ni kwa sababu ninatumia malimao machanga dozi ilipunguzwa hadi kufikia nusu kikombe. (Nusu kikombe cha juisi na kijiko kimoja cha asali mara tatu kwa siku). Kuharisha kulikoma. Na siku ya mwisho (Ya nne) nilimalizia dozi moja ya mwisho kukamilisha jumla ambayo ni mara tisa (9).
Na nilipona malaria.
Kupona kutokana na matumizi ya mchanganyiko huu inaweza kuwa labda ni faida ya chakula kikitumika vizuri kama dawa. Hivyo haitarajiwi kama inaweza kuwa na madhara makubwa sana (side effects).
Malimao hutumika katika mapishi mbalimbali (Katende na wenzie, 1995). Napia mchanganyiko wa malimao na juisi ni hutumika kwa ukawaida kuandaa nyama na samaki katika kile kinachoitwa 'marinating' (Malolo na wenzie, 2001).
Hata hivyo tuchukue tahadhari maana kuna usemi wa kiingereza usemao 'The safest medicine is only a useless one'. Uwezo wa dawa hii kuua vimelea vya malaria unatupa mwanya wa kufanya tafiti zaidi ili kuweza kupata dozi ambayo itaua wadudu tu bila madhara yeyote kwa mwili wa mwanadamu

Maumivu ya kichwa ambayo mara nyingi huambatana na homa ya malaria iliendelea kuwepo hadi siku ya pili na tatu za kutumia mchanganyiko wa dawa hii.

8. Hitimisho na mapendekezo
Kwa kukosa vifaa vya kisasa kuweza kufanya utafiti kimaabara. Msimuliaji anatarajia kuwa baadhi ya wasomaji wa utafiti/makala haya wataifanyia kazi kisayansi zaidi.

10. Maandishi ya kurejea
Tafiti ya kiingereza hapa I am my own guinea pig in malaria remedying
1. KATENDE,A.B,BIRNIE ANN; TEGNAS BO. (1995). Citrus limon Rutaceae. In : Useful Trees and Shrubs for Uganda
2. MALOLO,M.; MATENGA-SMITH,T.; TUNIDAU-SCHULTZ. J. 2001 Lemon Citrus limon In: The Fruits We Eat. SPC.CTA. Noumea, New Caledonia pp 46-49
Marejeo mengine

Soma kitabu chenye dawa zaidi hapa Ijue mimeadawa ya tiba na huduma ya kwanza

Waionaje tafiti hii (Maoni)
Sahili__ni rahisi na inaeleweka
Tata__ ni ngumu kueleweka
Nzuri__inafaa kwa ajili ya wanadamu
Maoni kwa ufupi

Matumizi ya malimao na athari zake katika kasi ya uondoshwaji wa vijidudu vya malaria na hali ya damu ya panya walioambukizwa P. berghei.

Muhtasari

Limao ni tunda litokanalo na mlimao. Mlimao hupatikana katika familia ya Rutacea katika kundi la Citrus, ni mmea uliosambaa ulimwenguni kote
Matunda haya hutumika kama chakula, kutia ladha, juisi na katika mapishi mbalimbali. Matumizi ya malimao hayakuishia hapo, watu huyatumia katika matibabu ya saratani, uzito (unene), pamoja na malaria ki-jadi.
Tafiti zimeonesha matokeo mazuri katika vipimo vya damu kutokana na matumizi ya limao au sehemu zake.Lakini hata hivyo baadhi ya wanajamii wamekuwa na imani ambayo haikuthibitishwa.
Katika utafiti mmoja matumizi ya juisi ya ndimu pamoja na dawa mseto za malaria yalipelekea matokeo mazuri katika matibabu ya malaria. Katika jamii malimao huchemshwa na kutumika katika matibabu ya malaria. Utafiti katika matumizi hayo ni wa kuripotiwa na mtu mmojammoja hivyo utafiti huu unaangazia uthabiti wa matumizi hayo.

Kusudi
Kuchunguza madhara ya malimao katika kupambana na malaria pamoja na athari zake kati hali ya damu kwa ujumla, utafiti uliofanywa kwa panya walioambukizwa vijidudu vya Plasmodium berghei.


4. Mamlaka
Mtafiti: Kelvin M. Shija
Mthibiti:Chuo cha afya na sayansi shirikishi MUHIMBILI (MUHAS)
Matakwa binafsi: Sina matakwa binafsi.

5. Mbinu na namna ulivyofanyika
Vipande vya limao vilikatwakatwa na kisha kuongezewa maji na kuchemshwa kwa muda wa dakika 45. Kila siku mchanganyiko mpya ulitengenezwa. Panya 25 walitumika katika utafiti huu.
Mtindo wa utafiti alioutumia Ryley na mwenzake Peters uitwao 'Kipimo cha matibabu cha Rane' ulitumika. Panya 20 waliambukizwa na malaria kisha baada ya muda waligawanywa katika makundi manne ya matibabu
1. Walipewa maji tu
2. Walipewa mchemsho wa malimao
3. Walipewa dawa mseto
4. Walipewa limao pamoja na dawa mseto
5. Hawa hawakuambukizwa wala kutibiwa (uangalizi)
Matibabu yalifanywa kwa muda wa siku nne. Vipimo vya malaria vilifanyika kila siku kwa siku tano. Damu ilipimwa kwa kuangalia wingi wa damu na seli nyinginezo kwa mashine maalumu. Kwa baadhi ya makundi wingi wa damu ulipimwa kwa kutumia njia rahisi ya mashine izungukayo.

6. Matokeo
Katika siku ya nne ya matibabu vipimo vilionesha kuwa; kwa wastani wadudu katika kundi lililopewa malimao walikuwa wachache (24%) ukilinganisha na kundi ambalo hawakutibiwa kabisa (40%)
Lakini kundi lililopewa dawa mseto ndilo halikuwa na wadudu kabisa (0%)
Siku za kuishi pia ziliongezeka katika kundi lililopewa malimao (siku 11) ukilinganisha na kundi ambalo hawakutibiwa (siku 8)
Katika vipimo vya damu hakukuwa na utofauti wa kutokana na matumizi ya malimao ulioweza kujipambanua kitakwimu
. Hata hivyo matumizi ya malimao kwa pamoja na dawa mseto yalipelekea kupunguza muda uliohitajika kuondosha asilimia 99% ya vijidudu vya malaria ukilinganisha na kutumia dawa mseto peke yake. (saa 58.8 vs saa 62.2). Tofauti hazikuonekana kuwa kubwa katika uzito wa panya kutokana na matumizi ya malimao

8. Mchanganuo na majadiliano
Utafiti huu japo umefanyika katika panya, lakini umeonesha matokeo yanayotufungua bongo katika matumizi ya malimao
Kuongezeka kwa kasi ya kuondoshwa kwa seli zilizoathiriwa na malaria kunasemekana kuwa msingi wa matokeo haya.
Ukihitaji maelezo zaidi utayapata katika utafiti kamili ambao utachapishwa siku za usoni

Lakini utafiti wa mtu mmoja (Nimejifanya mnyama wangu wa majar..) unaweza kuupata hapa Makala

Hitimisho
Mchemsho huu wa malimao umeonesha kuwa na vitu vinavyosaidia kufubaza malaria kwa asilimia 39% ukilinganisha na panya wasiopewa dawa. Lakini haikutosha kuleta uponyaji kabisa mchemsho ulipotumika peke yake, malimao hayakuwakinga panya na upungufu wa damu utokanao na malaria. Lakini mchemsho wa malimao huohuo ulipotumika pamoja na dawa mseto matokeo mazuri zaidi yalipatikana kwa upande wa uondoshaji wa haraka wa vijidudu vya malaria na hali nzuri ya damu na kinga kwa ujumla.

9. Mapendekezo
Utafiti zaidi ufanyike kwa binadamu waishio maeneo yenye malaria (endemic) ili kuondoa tofauti zilizopo kati ya viumbe na namna asili ya ugonjwa ulivyo. Tafiti katika panya zina changamoto nyingi.

10. Maandishi ya kurejea
Utangulizi wa kiingereza hapa Abstract; Effect of lemon decoction on malaria parasite clearance and selected hematological parameters in plasmodium bhergei infected mice.
Marejeo mengine
1. Marejeo yapo katika utafiti mwenyewe


Waionaje tafiti hii (Maoni)
Sahili__ni rahisi na inaeleweka
Tata__ ni ngumu kueleweka
Nzuri__inafaa kwa ajili ya wanadamu
Maoni kwa ufupi

Upandaji wa nafasi tofautitofauti kwenye zao la beetroot(Beta vulgaris) ili kulinganisha matokeo ya zao hilo katika ukuaji na mavuno.

Muhtasari

Ili kupata mavuno bora kabisa inahitajika kutumia kanuni za kilimo bora. Katika kilimo bora upandaji wa nafasi inayo stahili ni muhimu kuzingatiwa.

Kusudi
Tafiti kuona athari za kutumia nafasi tofautitofauti katka upandaji wa zao la beetroot, katika ukuaji na mavuno ya beetroot.

4. Mamlaka
Mtafiti: Anold Lameck Steward
Mthibiti:Chuo kikuu cha kilimo Sokoine (SUA)
Matakwa binafsi: Hakuna matakwa binafsi yaliyobainishwa

5. Mbinu na namna ulivyofanyika
Kuotesha zao la beetroot kwa kutumia nafasi tofautitofauti kama ifuatavyo
i. 15cmx10cm
ii. 30cmx10cm na
iii. 45cmx10cm
katika shamba la majaribio

6. Matokeo
Beetroot iliyo pandwa katika nafasi ya 45cmx10cm ilifanya vizuri Zaidi katika ukuaji na mavuno kulinganisha na nafasi zingine ambazo ni 15cmx10cm na 30cmx10cm hii ni kwa sababu nafsi 45cmx10cm inapelekea zao hilo utanuzi mkubwa wa kinundu cha mzizi wa mmea katika ukuaji na kupelekea ukuaji wa mmea wenyewe kwa kuupa uwazi mkubwa wa mmea kujitengenezea chakula chake

8. Mchanganuo na majadiliano
Katika utafiti uliofanywa juu ya upandaji wa nafasi tofautitofauti ( 15cmx10cm, 30cmx10cm na 45cmx10cm) , kwenye zao la beetroot ili kulinganisha matokeo ya zao hilo katika ukuaji na mavuno katika chuo kikuu cha kilimo Sokoine. Hivyo basi beetroot iliyo pandwa katika nafasi ya 45cmx10cm ilifanya vizuri zaidi katika ukuaji na mavuno kulinganisha na nafasi zingine ambazo ni 15cmx10cm na 30cmx10cm hii ni kwa sababu nafsi 45cmx10cm inapelekea zao hilo utanuzi mkubwa wa kinundu cha mzizi wa mmea katika ukuaji na kupelekea ukuaji wa mmea wenyewe kwa kuupa uwazi mkubwa wa mmea kujitengenezea chakula chake na kupelekea beettroots zinazo zalishwa kuwa bora, kupata mavuno mazuri kwa wingi zaidi na kupata masoko.

Hitimisho na Pendekezo
Hivyo basi wakulima wa Tanzania wanashauriwa kutumia nafasi 45cmx10cm katika uzalishaji wa zao la beetroot ili kupata mavuno mazuri pamoja na masoko ili kuendeleza uzalishaji wa zao la beetroot.

10. Maandishi ya kurejea
Utangulizi wa kiingereza unapatikana hapa Abstract; Effect of planting spacing on the growth and yield of beetroot (Beta vulgaris).


Waionaje tafiti hii (Maoni)
Sahili__ni rahisi na inaeleweka
Tata__ ni ngumu kueleweka
Nzuri__inafaa kwa ajili ya wanadamu
Maoni kwa ufupi

Uchunguzi wa uelewa na ufanyaji wa uchunguzi binafsi wa matiti kati ya wanafunzi wa kike katika Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili.

Muhtasari

Ugundulikaji wa haraka wa kansa ya matiti kwenye jamii kupitia program ya uchunguzi binafsi wa matiti umekuwa muhimu katika kupunguza kansa na vifo vitokanavyo na kansa ya matiti. Uchunguzi binafsi wa matiti umekuwa njia nzuri ya kuepusha vifo hivyo kwa sababu husaidia kugundua na kutibu mapema.

Dhumuni
Kuchunguza uelewa na ufanyaji wa uchunguzi binafsi wa matiti kati ya wanafunzi wa kike ngazi ya Shahada katika Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili.

4. Mamlaka
Mtafiti: Agripina Gotfrid Massawe
Mthibiti:Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)
Matakwa binafsi: Sina matakwa binafsi

5. Mbinu na namna ulivyofanyika
Tafiti hii iifanyika kati ya mwezi Disemba, 2017 na mwezi wa tatu, 2018 kati ya wanafunzi 101 wa kike ngazi ya shahada katika Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Dar es Salaam, Tanzania. Maswali 15 mafupi yaliyoandaliwa na kupewa kwa washiriki yalitumika kukusanya taarifa binafsi ,uelewa na ufanyaji wa uchunguzi binafsi wa matiti. Pia wanafunzi waliangaliwa namna wanavyojifanyia uchunguzi wa matiti wenyewe na taarifa zao zilijazwa katika fomu maalumu iliyoandaliwa.

6. Matokeo
Jumla ya wanafunzi 101 walishiriki kwenye tafiti.Wengi 67 (66.3%) walikuwa na uelewa mkubwa,28 (27.7%) walikuwa na uelewa wa kati na 6 (5.9%) walikuwa n uelewa mdogo na wengine hawakuwa na uelewa kabisa kuhusu uchunguzi Binafsi wa matiti.5(5%) walikuwa na ufanyaji mzuri,46 (45.5%) walikuwa na ufanyaji wa kati na 50 (49.5%) hawakujua kufanya uchunguzi wa matiti.Hakukuwa na uhusiano kati ya uelewa na ufanyaji wa uchunguzi binafsi wa matiti na hii ilithibitishwa na thamani ya P=0.287 katika mwendano wa asilimia 95.

7. Hitimisho na Pendekezo
Ili kuimarisha ufanyaji wa uchunguzi binafsi wa matiti, ni muhimu kuhakikisha kuwa wafanyakazi wa afya kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali wanaimarisha mazingira ya kazi pamoja na kuwaelimisha wanawake katika umuhimu wa kufanya uchunguzi binafsi wa matiti katika nchi yetu, Tanzania.

8. Maandishi ya kurejea
Utangulizi wa kiingereza unapatikana hapa Abstract; Assessment of Knowledge and Practice of Breast Self-Examination Among Female Undergraduate Student at MUHAS, Dar es Salaam, Tanzania.Waionaje tafiti hii (Maoni)
Sahili__ni rahisi na inaeleweka
Tata__ ni ngumu kueleweka
Nzuri__inafaa kwa ajili ya wanadamu
Maoni kwa ufupi

Mfano; Matumizi ya mmea xxxx kwa matibabu .
Hata hivyo ukiona njia hii ni ngumu kwako. Tuma vitu viwili tu (1) Makala ya kiswahili na (2) PDF ya utafiti wako. Kwa pamoja.

2. Utangulizi
Tatizo la homa ya malaria limekuwa likisumbs
Tafiti zimeonesha ongezeko la usugu...... Ninafanya utafiti huu kuangalia uwezekano wa matibabu.....Eleza kiufupi kuhusiana na tatizo unalolifanyia kazi

3. Malengo na kusudi
(a)Kuona ubora na usalama wa mmea ujulikanao kama mmmm nnnn
(b)Kupima.........
(c)__________

4. Mamlaka
Mtafiti:Jina a, jina b na Mtafiti Tata
Mthibiti:Binafsi / Chuo cha .....(Taasisi unayofanya kazi chini yake)...MUHIMU
Matakwa binafsi: Sina matakwa binafsi.
Mengineyo: Namshukuru tu mungu, na rafiki yangu....(kama yapo).

5. Mbinu na namna ulivyofanyika
Njia ya kutafuta katika vitabu na mtandao(kwa watafiti binafsi inatosha)
Mbinu nyingine za kisayansi na kijamii
Maabara (Kisha eleza vifaa na mbinu kwa kiswahili rahisi lengo mtu apate ile picha inayoeleweka)

6. Matokeo
Majedwali na michoro ihusike. Isiwe tata sana bali iwe sahili tu.

8. Mchanganuo na majadiliano
Maelezo ya kutosha kuelezea maana ya kile ambacho utafiti umeonesha ....
Maelezo haya yasizidi sana na yatokane na utafiti huu tu
Lakini kama utahitaji kuelezea zaidi kiujumla zaidi. Andaa kazi katika mtindo wa makala na itume. Kutakuwa na kitufe cha soma zaidi hapa kama hiki
Soma zaidi hapa Makala yake.

8. Hitimisho
Andika hitimisho la utafiti kwa sentesi chache tu
9. Mapendekezo
Mapendekezo yako

10. Maandishi ya kurejea
Tafiti ya kiingereza hapa The efficacy of plant xxx mmm in the treatment of malaria.
Marejeo mengine
1. MAHUYEMBA, A.S. (2013). Ijue mimeadawa ya tiba na huduma ya kwanza. Toleo la 1
https// www.example.com iliyotembelewa siku ya Juni 7 2017 (mtandao ulikopata data)
https// www.example.com iliyotembelewa siku ya Juni 7 2017 (mtandao ulikopata data)

Soma zaidi hapa (eng) Utafiti wa kisayansi (viungio kwenda moja kwa moja katika kurasa muhimu)

Waionaje tafiti hii (Maoni)
Sahili__ni rahisi na inaeleweka
Tata__ ni ngumu kueleweka
Nzuri__inafaa kwa ajili ya wanadamu
Maoni kwa ufupi

Kiwango cha wadudu na kemikali katika mfumo wa maji daressalaam
Inapakiwa
Soma zaidi hapa (eng) The amount...

Waionaje tafiti hii (Maoni)
Sahili__ni rahisi na inaeleweka
Tata__ ni ngumu kueleweka
Nzuri__inafaa kwa ajili ya wanadamu
Maoni kwa ufupi

Chapisha utafiti wako katika ukurasa huu
Wasilisha kazi kupitia ukurasa huu. Bofya kiungio cha wasilisha hapo wasilisha


Taarifa zilizo katika mtandao huu hazilengi kuwa mbadala wa taarifa rasmi kutoka katika vyombo vyenye mamlaka kama, daktari au mtoa huduma ya afya. Au sekta yoyote rasmi. Taarifa na habari hizi ni kwa ajili ya ujuzi tu.