makala sahili

LoGo

Virusi sio viumbe wa ajabu, ni taarifa tu !

Kelvin Mashauri


Viruses are nothing but pieces of information !Taarifa, maana na uhalisia wa virusi - Information meaning and reality of viruses!
Tangu kugundulika kwake, virusi vimewaacha midomo wazi wanasayansi na wanataaluma kutokana na uajabu wake. Maajabu yake yapo katika kukosa kwake sifa kadhaa ambazo kiumbe hai anapaswa kuwa nazo. Na hata sasa hakuna muafaka yakuwa ni kiumbe hai ama si kiumbe. Tafsiri yake imebaki kuwa ‘Kirusi ni kipande kidogo sana chenye jeni (chembeurithi) iliyozungukwa nap rotini, vipande hivi huambukiza seli na kuzaliana katika seli husika.
Kama inavyofahamika kwamba kwamba jeni ndicho kitu pekee kinachoweza kuhamisha na kutunza taarifa katika viumbe hai. Na muundo wake ni tata sana, sana.. sana. Basi tunaweza kusema kwamba virusi ni vipande vya taarifa kutoka katika seli moja kwenda kwenye nyingine. Au kutoka kwa kiumbe mmoja kwenda kwa kiumbe mwingine.

Taarifa
Ni ujumbe kutoka upande mmoja hadi mwingine. Ujumbe huu huweza kuwa ndio umezalishwa na huyo anayetuma ama yeye anasambaza kile tu alichoambiwa ama kusikia.
Tunasambaza taarifa za hatari kwa haraka zaidi ili wapendwa wetu wachukue tahadhari
Taarifa nyingine huweza kuwa maarufu kiasi kwamba ni kila mtu anajua hivyo na anatenda kulingana na ujumbe husika.
Wakati mwingi tunasambaza taarifa bila kuulizwa nahiyo ni ili kuwalinda tunaowapenda na wanaotuzunguka, tunahisi ni jukumu letu kabisa.
Basi kutokana na hayo tuliyoyaona na tunayoyafanya kiasili kabisa ndivyo seli zetu hufanya vivyo hivyo. Pale seli inapohisi ina taarifa ya muhimu kuwafikishia seli nyingine inaweza kutumia baadhi ya njia zifuatazo;
Kutumia mnunurisho, kwa kuzalisha mawimbi ya umeme au sauti au miali yoyote yenye uwezo huo. Mfano seli za neva.
Kutumia molekyuli ndogo au kemikali rahisi kama sodiamu au kalisiamu. Kwa mfano misuli.
Kuzalisha kemikali tata za protini mafuta au viungo vingine. Kwa mfano estrojeni na thairoksini.
Kutumia jeni zenye taarifa husika. Mfano bakteria wanavyofundishana usugu kwa kupitia plasmidi
Njia ya mwisho haitumiki sana katika mawasiliano ya kawaida. Bali hutumika katika mawasiliano ya muhimu na ya siri. Kama vile kujilinda na hatari inayozikabili seli za jamii husika. Seli za jamii husika zinaweza kuwa katika kiumbe huyohuyo au kwa kiumbe mwingine. Na vipande vya taarifa hizo ndizo huitwa virusi. Nitasema hivyo kwa mifano:

Mafua
Maambukizi ya virusi katika njia ya hewa husababisha kutokwa na mafua mepesi. Kuna namna nyingine za mafua zitokanazo na sababu nyingine lakini tutaongelea haya yatokanayo na virusi.
Mafua haya husambaa kwa kasi wakati wa baridi. Wakati huu ambapo hewa huwa ya baridi na kavu ndipo hasa msimu wake.
Ifahamike kuwa hewa ya baridi sana huumiza njia ya hewa (Ndiyo maana kuna asthma). Hewa kavu vivyo hivyo. Kwa kawaida hewa hupita puani kupatiwa unyevu na joto lifaalo kabla ya kufika kwenye mapafu.
Ni muhimu basi kuwa na maji/unyevu wa kutosha wakati huo ili kuwezesha hayo. Na seli inayopata taarifa hii ama kwa kuianzisha, au kusikia huona ni vyema kuwajulisha wenzake. Na kwa kuwa taarifa hii inapaswa kuwa mahsusi na itapita maeneo mengine mengi basi huwekwa katika mfumo wa siri (code) kisha kusambazwa.
Seli nyingine itakayopokea hutumia na kufanya vivyo hivyo! Na taarifa/mafua/kirusi husambaa kirahisi.

Virusi vinavyohusishwa na kansa/saratani
Kuna swali watu hujiuliza iwapo kansa huambukiza? Je kansa huweza kutoka kwa mgonjwa mwingine kwenda kwa mwingine, jibu ni hapana na ndiyo.
Kansa ni mwitikio wa seli kujilinda na hali ngumu ya kimaisha kama kemikali au miali mikali. (Soma zaidi hapa Saratani.) Virusi hivi hutumika kutoa taarifa kwa seli nyingine ili ziige mfano wa kujizalisha. Sasa itategemea na hizo seli nyingine. Zikihisi hakuna matatizo au mazingira magumu zitapuuzia. Endapo zikihisi kuna ulazima wa kukua(kujiongeza) basi zitafanya hivyo. Kwa mfano Human papiloma virus (HPV). Umri mdogo kuanza kufanya mapenzi na idadi ya wanaume imetajwa kuwa chanzo kwa mwanamke husika. Lakini mwanamke anaweza kupata taarifa/virusi kutoka kwa mwanaume wake na kupata kansa ya uzazi.

Mwisho kama ilivyo kwa taarifa nyingine, basi wapo watu wanaozipokea na kufanyia kazi, wengine hupuuzia. Wengine huamua kuzibadili, taarifa nyingine ni za uongo. Vivyo hivyo na virusi, watu wengine hawaugui hata wapatapo virusi. Na si rahisi kurudia tena kufanyia kazi taarifa ambayo tayari unaujua mwisho wake kuwa si hatari na ndiyo maana kuugua mara mbili kirusi wa aina moja sio kawaida sana. Angalau kwa muda mfupi, lakini endapo umepita muda mrefu tangu kupata virusi/taarifa fulani basi kuna uwezekano wa kuugua tena. Kuugua mafua mara mbili katika msimu mmoja si kawaida.
-Mashauri

Waionaje makala hii (Maoni)
Sahili__ni rahisi na inaeleweka
Tata__ ni ngumu kueleweka
Nzuri__inafaa kwa ajili ya wanadamu
Maoni kwa ufupi

Taarifa zilizo katika mtandao huu hazilengi kuwa mbadala wa taarifa rasmi kutoka katika vyombo vyenye mamlaka kama, daktari au mtoa huduma ya afya. Au sekta yoyote rasmi. Taarifa na habari hizi ni kwa ajili ya ujuzi tu.